
Jamii imeshauriwa kuacha
kuwatumia watoto wadogo kama chanzo cha kujipatia kipato katika familia na
badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza watoto ambao wanaishi na
kufanya kazi mitaani.
Hayo yamesemwa na
afisa ustawi wa jamii na mratibu wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani
kutoka shirika lisilo la kiserikali KISEDET mkoani Dodoma Bwana Ibrahim Mtangoo
alipokuwa akizungumza na Dodoma FM ambapo ameitaka jamii kuacha kuwatumia
watoto kama chanzo cha maendeleo kwa kufanya hivyo ni kinyume na haki za
watoto.
Bwana Mtangoo amesema
kuna baadhi ya wazazi wanawatuma watoto kwenda kuomba fedha ambapo baadhi ya
watoto wamethibitisha suala hilo na kuitaka jamii inayosaidia watoto hao kuacha
kutoa fedha badala yake wawapatie chakula.
Watanzania
wametakiwa kuelewa kuwa suala la kufanya kazi kwa bidii ni jukumu la kila mtu
ili kupiga vita dhidi ya umaskini kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza idadi
ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Na
Benard Filbert Dodoma fm
Comments
Post a Comment