
Mkuu wa mkoa wa Dodoma
DR.BINILITH MAHENGE amewataka TARURA pamoja na wakandarasi kutumia fedha
walizopewa ipasavyo katika matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/18
na kuwashirikisha wananchi wa maeneo
husika katika miradi hiyo ili kutunza miundombinu.
Ameyasema hayo
wakati wa Zoezi la utiaji saini mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara kupitia TARURA ambao ni wakala wa barabara za mjini na vijijni na wakandarasi iliyofanyika jana katika ukumbi wa VETA kwa
awamu ya pili kwa lengo la kuanza matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha
2017/18.
DR MAHENGE Amewahimiza
wakandarasi waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo kutengeza barabara kwa
kiwango kilicho bora ili kuendelea kuimarisha miundombinu hapa nchini.
Mratibu meneja
wa TARURA mkoani Dodoma Bwana
MOHAMAEND MKWATA amesema kazi kubwa ya TARURA
ni kuendelea kufanyia matengenezo mtandao wa barabaraza za mijini na vijijni
na Utekelezaji wa miradi hiyo
ukizingatia mpango wa manunuzi na uwepo wa fedha kwa kuzingatia miradi husika.
Katika awamu ya
kwanza TARURA mkoa wa Dodoma imeweza kufanikinikisha kusainiwa kwa mikataba
ishirini na saba katika halimashauri za Bahi,Chamwino ,Kongwa na Dodoma Manispaa
huku miradi 25 ikifanyiwa mchakato wa manunuzi
Katika awamu ya
pili matengenezo yanatarajiwa kufanyika katika wilaya ya Mpwapwa,Chemba,Kondoa,pamoja
na manispaa ya Dododma.
Na
Mindi Joseph Dodoma Fm
Comments
Post a Comment