MANISPAA YA DODOMA YAOMBWA KUHARAKISHA ZOEZI LA UPIMAJI WA MITAA ILI SHUGHULI ZA MAENDELEO ZIENDELEE
Imeelezwa
kuwa kuchelewa kwa upimaji wa mitaa ndani ya manispaa ya Dodoma kunachangia
kukwama kwa nguvu kazi kutoka kwa wananchi katika kujitolea kuboresha miundombinu
mibovu katika baadhi ya mitaa .
Hayo yameelezwa na
mwenyekiti wa mtaa wa chinyoya kata ya kilimani
manispaa ya Dodoma Bi FAUSTINA
BENDELA wakati akizungumza na Dodoma FM ambapo amesema kuwa changamoto zinazoukabili mtaa wake zinasababishwa
na kuchelewa kwa zoezi la upimaji wa mitaa.
Amesema zipo
barabara mbovu na mifereji iliyoziba lakini uwawia vigumu wananchi kuweka nguvu
kazi kwani bado mtaa huo haujapimwa na zoezi hilo linasimamiwa na halimashauri
ya manispaa ya Dodoma licha ya awali mtaa huo kuwa chini ya mamlaka ya
ustawishaji makao makuu CDA.
Aidha Bi FAUSTINA
ameiomba halimashauri ya manispaa ya Dodoma kulichukulia uzito suala hilo la
upimaji wa mitaa kwani uwepo wa miundombinu mibovu unasababisha kukwama kwa
baadhi ya shughuli za maendeleo.
Katika hatua
nyingine akizungumzia suala la ulinzi na usalama mwenyekiti huyo amesema kwa
sasa hali ni shwari huku akimpongeza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Dodoma GILLES MUROTO kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa
wenyeviti wa mitaa pale anapoombwa msaada.
Hata hivyo
amewaomba wananchi wa mtaa wa chinyoya kuendelea kuitikia wito wa mikutano ya
hadhara inayoitishwa kwa ajili ya kujadili maendeleo ya mtaa wao.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA
FM
Comments
Post a Comment