Katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu manispaa ya Dodoma imeandaa mkakati mpya wa kuhakikisha kila mtu anayeingia hospital anapimwa ugonjwa huo.
Hayo
yamebainishwa na mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu manispaa ya Dodoma Dokta
Pelesi Lukango wakati akizungumza na dodoma FM kupitia kipindi cha taswira ya
habari ambapo amesema tayari wameandaa fomu za usajili kwa kila eneo la
hospitali kuhakikisha kila mgonjwa anayeingia anapimwa afya yake.
Hata hivyo
dokta peles amesema kwa sasa changamoto ni kubwa ambapo kila mgonjwa anayeugua
kifua kikuu hubainika na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Amewataka
wananchi kuhakikisha wanaenda kwenye vituo vya afya kupima na kutambua afya zao
ambapo huduma hizo hutolewa bure bila malipo.
Hivi
karibuni waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh,Ummy
Mwalimu alinukuliwa akisema kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO takwimu
zinaonesha kuwa watu 77 hufariki dunia kila siku nchini Tanzania kutokana na
kifua kikuu huku mkoa wa Dar –Es-Salaam
ukitajwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 20.
Na Benard Filbert Dodoma
FM
Comments
Post a Comment