Serikali kupitia wizara ya
ujenzi uchukuzi na mawasiliano imesema itaendelea kuwezesha mamlaka ya hali ya
hewa nchini kwa kutenga bajeti ya kutosha ili kukabiliana na changamoto
zilizopo katika mamlaka hiyo.
Waziri wa ujenzi
uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi
wa baraza ya wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania leo mjini Dodoma
ambapo amesema serikali inatambua mchango wa mamlaka ya hali ya hewa hivyo
itaendelea kuwezesha kuinua mtandao wa vituo vya mamlaka hiyo.
Prof.Mbarawa
amesema mamlaka ya hali ya hewa imekua ikitoa mchango katika taifa na kwamba
mamlaka hiyo imejenga kuaminika kwa
wananchi kutokana na taarifa zake zinatolewa na kuwataka kuongeza juhudi katika
ufanyaji kazi wao ili waaendelee kuaminika.
Awali akisoma hotuba
mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Dr Agnes Kijazi amesema
licha ya kuwepo kwa mafanikio katika mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na Tanzania
kuwa nchi ya tatu barani Afika kupata cheti cha ubora bado wana uhitaji wa
kubadilisha vifaa vinavyotumia zebaki ifikapo mwaka 2020.
Mariam
Matundu
Dodoma FM
Comments
Post a Comment