
Imeelezwa kuwa madaktari bingwa
wa magonjwa mbalimbali hapa nchini wamekubaliana kushirikiana na madaktari
kutoka nchini Palestina katika kuimarisha matibabu ya kibingwa kwenye hospitali
mbalimbali hapa nchini ili kutoa huduma bora kwa watanzania.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar –es-Salaam na waziri wa afya na maendeleo ya jamii jinsia wazee na
watoto mh Ummy Mwalimu wakati wa kutia saini makubaliano ya kuboresha mifumo ya afya nchini kati ya
serikali ya Tanzania na serikali ya Palestina.
Aidha waziri Ummy amesema
kuwa serikali kupitia makubaliano hayo wamekubaliana kuleta madaktari bingwa wa
kutibu mifupa ya uti wa mgongo na fahamu kwani nchi hiyo ina wataalamu wengi wa
magonjwa hayo
Kwa mujibu wa
waziri Ummy amesema kuwa licha ya kufikia asilimia themanini katika upatikanaji
wa dawa nchini makubaliano hayo pia yatalenga kuimarisha uzalishaji wa dawa
pamoja na chanjo hasa za magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari,shinikizo la
damu na saratani kwani vinaongeza idadi kubwa ya vifo hapa nchini.
Kwa upande wake
balozi wa serikali ya taifa la Palestina Bwana Hazem Shabat amesema kuwa
wamefurahishwa kuingia mkataba huo na serikali ya Tanzania kwani wanahitaji kwa
nia ya dhati kuisaidia sekta ya Afya hapa nchini.
Na Rweikiza
Katebalirwe & Alfred Bulahya
Dodoma FM
Comments
Post a Comment