Maafisa ustawi wa
jamii ngazi ya mkoa na halmashari wametakiwa kushirikiana na maafisa ustawi wa
jamii ngazi ya kata ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya utekelezaji wa sera
mbalimbali zinatomtaka mwanaume kutimiza wajibu wake katika familia.
Msemaji wa wizara
ya afya maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto idara kuu ya maendeleo ya
jamii Erasto Ching’oro amesema ipo haja kwa maafisa ustawi wa jamii kuendelea
kutoa elimu kwa jamii hususani wanaume kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Amesema kwa mujibu
wa sheria ya ndoa sura ya 69 katika kifungu cha 63A kimempatia wajibu mwanaume
wa kutunza familia yake kikamilifu na iwapo atapata matatizo ya kiafya busara
na maridhiano katika familia yatafanyika ili kuendelea kuimarisha familia.
Amesema mbali na
sheria hiyo ya ndoa ,sera ya maendeleo ya jinsia ya mwaka 2000 imesisitiza
wajibu wa mwanaume katika kushirikiana na mwanamke ili kutunza familia
kikamilifu.
Hata hivyo wazazi
wote wametakiwa kutambua jukumu la kutunza familia kwa kutoa malezi bora kwa
wototo wote pasipo kubagua jinsia ni jambo linalowezesha kuwa na familia bora.
Mariam
Matundu Dodoma FM
Comments
Post a Comment