Watendaji wa kata pamoja na wataalamu wa afya
wametakiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya kujilinda na magonjwa yatokanayo na uchafu
wa mazingira.
Wito huo umetolewa
na Afisa Afya wa Manispaa ya Dodoma Bw.ABDALA MAHIYA wakati akizungumza na
kituo hiki ambapo amesema tayari wamewaagiza watendaji kata mbalimbali mkoani
hapa kutoa elimu kwa jamii lengo likiwa ni kuondoa aibu ya kuugua magonjwa
yanayoweza kuepukika.
Aidha amesema kuwa
sehemu za hotelini na migahawani ndizo zinazotakiwa kupewa elimu zaidi kutokana
na mazingira yao ya kazi kuwa hatarishi kwa afya za wananchi wengi kwakuwa
wanapoharibu wao watu wengi wataathirika tofauti na kaya moja.
Ameongeza kuwa
elimu wanayotakiwa kupewa ni kuweka maji ya moto kwaajili ya kunawia mikono
pamoja na kufunika chakula vizuri ili kuzuia vimelea vya magonjwa kuweza
kushambulia vyakula na kuleta madhara kwa watumiaji.
Sanjari na hayo
wananchi pia wameshauliwa kusimamia usafi mwenyewe katika eneo lake na
kuhakikisha anatumia maji safi na salama ambayo yametibiwa na dawa ya wotagadi.
Na
ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment