KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI MJINI DODOMA KUANZIA KESHO KITAKUWA RASMI KATIKA KITUO KIPYA CHA NANE NANE NZUGUNI
Zoezi la uhamishaji wa Kituo cha Mabasi mkoani Dodoma linatarajiwa kukamilika kwa siku ya leo huku madereva ,abiria na wafanyabiashara wakilalamikia miundombinu ya kituo kipya.
Wakizungumza na Dodoma FM mapema leo baadhi ya wafanyabiashara
wamesema stendi ya Nanenane haiwafai kutokana
na miundombinu kutoridhisha hali ambayo imepelekea kupangiwa muda wa kufunga
kufanya biashara zao.
Nao Madereva wa mabasi wameeleza kuwa stendi ya Nanenane
bado ni changamoto kwao kwa sababu baadhi
ya gari zitakuwa zinabeba abiria wote katika stendi ya Sabasaba na kupelekea wao kukosa abiria.
Hata hivyo baadhi ya abiria wamesema kutokan na kuhamishwa
kwa stendi ya mkoa watakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa gharama ya usafiri kutoka mjini
hadi stendi ya Nanenane.
Dodoma FM imezungumza na Afisa habari wa manispaa ya Dodoma Bwana
RAMADHANI JUMA ambae amekiri kuwa leo ni siku ya mwisho kuhamishwa stendi hiyo na kwamba kuanzia kesho shughuli zote za usafiri zitapatikana
katika eneo la Nanenane Nzuguni.
Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara,abiria na madreva
kuwa wavumilivu kwani ni kipindi cha mpito
na tayari manispaa inatarajia
kuanza ujenzi wa stendi ya kisasa eneo la NZUGUNI pamoja na soko kubwa ambapo itachukua miaka
miwili kukamilika.
Na,Mindi Joseph DODOMA FM
Comments
Post a Comment