![]() |
Wakati zoezi la usajili na
utambuzi wa watu likiendelea mkoani Dodoma juu ya kupatiwa vitambulisho vya
Taifa, wananchi wameombwa kutoa ushirikiano kuwabaini viongozi wanaowatoza watu
fedha kupata fomu.
Hayo yamebainishwa
na Afisa usajili mkoa wa Dodoma bwana Halidi Mrisho wakati akiongea na Dodoma
Fm katika mahojiano maalumu, ambapo amewataka watu kutoa ushirikiano kuwabaini
viongozi wa seriklai za mitaa wanaowatoza watu fedha kupata fomu za usajili, na
kuongeza kuwa fomu hizo hutolewa bure.
Aidha Bwana Mrisho
amewakumbusha watu kutoa pingamizi la kutopatiwa kitambulisho cha Taifa kwa mtu
ambaye siyo raia wa Tanzania au kwa walie na mashaka naye juu ya uraia wake kwa
kufika katika ofizi za serikali za mitaa au ofisi za NIDA zilizopo mkoani
Dodoma.
Hata hivyo wananchi
wametakiwa kuacha kudurufu fomu watakazopewa badala yake kama zitakuwa zimeisha
katika ofisi za serikali za mitaa watoe taarifa ili wapatiwe fomu nyingine.
Na
Victor Makwawa Dodoma Fm
Comments
Post a Comment