Wakazi wa kata ya
Majengo Manispaa ya Dodoma wametakiwa kuendeleza zoezi la usafi wa mazingira ili
kuepuka mlipiko wa magonjwa.
Rai hiyo imetolewa
na Katibu Tawala wa wilaya ya Dodoma Bi Humbi Ziota wakati wa zoezi la kufanya usafi
katika kata hiyo mwishoni mwa wiki.
Bi Humbi amemuagiza
diwani wa kata hiyo kuhakikisha kila mtaa ndani ya kata hiyo una vifaa vya
kutosha ili kurahisisha zoezi la usafi wa mazingira.
Aidha katibu huyo amewasisitiza
watendaji na wenyeviti wa mitaa mikoani Dodoma kuhakikisha wanasimamia zoezi
hilo ili kuweka mazingira safi nyakati zote.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bwana Godwin Kunambi akizungumza mara baada ya
zoezi la usafi amewapongeza viongozi wa mtaa huo kwa kutatua kero za wananchi
katika mikutano yao huku akisema kila eneo analoenda kero kubwa ni suala la
viwanja.
Wakati huo huo Bwana kunambi amewataka wakazi wa eneo hilo
kuhakikisha wanapaka rangi bati za nyumba ili kuboresha muonekano kuendana na hadhi
ya makao makuu.
Na
Benard Filbert Dodoma
FM
=
= = = = = = = = = = =
= = = = == = =
Comments
Post a Comment