Jamii yatahadharishwa juu ya kwenda
na mtoto sehemu za starehe ambazo zitaathiri ukuaji wake.
Tahadhari hiyo
imetolewa na mwanasheria Goodluck Ludala kutoka katika kituo cha Amani na
msaada wa kisheria mjini Dodoma wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya Umuhimu
wa wazazi kuwaepusha watoto kwenda katika kumbi za starehe.
Bwana Ludala amesema
sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imeweka mipaka katika sehemu za kustarehe ambapo sheria
ya mtoto namba 21 kifungu cha 17 imezuia wazazi ama walezi na wamiliki wa kumbi
za starehe kuruhusu watoto kufika katika kumbi hizo iwe ni kwa muda wa mchana
au usiku.
Aidha ameitaka
jamii kuacha mazoea kwa kufumbia macho vitendo vinavyoendelea katika jamii kwa
kuwatuma watoto vilevi kwani kutokutoa taarifa ni kuvunja sheria na unaweza
kutiwa hatiani.
Sheria ya mtoto ina
tafsiri mtoto kuwa ni mtu alie chini ya umri wa miaka 18 na inatoa wajibu kwa
kila mtu kumlinda mtoto pamoja na kutimiza haki zake zote za msingi .
Na
Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment