Wanajamii wameshauriwa kuacha kuhusisha
ugonjwa wa ukoma na imani za kishirikina hali inayoweza kupelekea kuenea kwa
ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa.
Rai hiyo imetolewa na
doctor Martin Masimba ambaye ni mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na ukoma
mkoani Dodoma wakati akizungumza na Dodoma
fm kupitia kipindi cha Taswira ya habari.
Dokta Masimba amesema
kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihusisha baadhi ya
magonjwa na imani za kishirikina huku wakiufanya ugonjwa huo kukua
zaidi.
Akizungumzia hali ya
ugonjwa wa ukoma mkoani Dodoma dokta Masimba amesema kuwa maambukizi ya ugonjwa
huo yamepungua tofauti na kipindi kilichopita,kutokana na jitihada
zinazoendelea kufanywa na wizara husika.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakizungumza na kituo hiki wamesema
baadhi ya watu huhusisha imani za kishirikina na ugonjwa huo baada ya kushindwa
kupona wanapotumia dawa za hospitali.
Kwa
mujibu wa shirika la afya duniani Takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha
mwaka 2015 kumekuwepo na maambukizi mapya ya Ukoma 212, 000 sehemu mbali mbali
za dunia, lakini asilimia 60% ya waathirika wote walikuwa wanatoka nchini
India Brazil na Indonesia takwimu
zingine ni kwamba, watoto walioambukizwa Ukoma ni asilimia 8.9% ya wagonjwa
wote duniani na kwamba, asilimia 6.7 ya watoto wagonjwa walionesha mabaka
mwilini wao!
Na Benard Filbert Dodoma FM
Comments
Post a Comment