Zaidi ya wateja mia nne
wamefungiwa mita za malipo kabla kutoka
idara ya maji DUWASA baada ya kukamilisha majaribio ya mita zitakazofaa kwenye matumizi
kwa njia ya mfumo huo.
Hayo yamesemwa na
mkuu wa kitengo cha mawasiliano DUWASA Mkoani Dodoma bwana Sebastian Warioba
wakati akizungumza na Dodoma FM ambapo amesema kuwa mpango huo ulianza mwaka
jana kwa kuzijaribu mita za makampuni
sita ikiwemo kampuni ya Joi.
Bwana Warioba amesema
baada ya majaribio hayo kampuni hiyo ilishinda na hivyo kuanza kutumika kwa
mita zake japo mita hizo zina bei kubwa zikigharimu dola mia tatu hadi mia tatu
hamsini kwa kila moja.
Bwana warioba amesema
lengo la kufunga mita kabla ya malipo ni kurahisisha upatikanaji wa maji kwa
mteja kama zilivyo mita za awali na kuwa mfumo huu utakuwa endelevu kwani
tayari unatumiwa na nchi nyingine duniani.
Aidha ametoa onyo
kwa wananchi wanaotumia maji bila uhalali na kubainisha kuwa wapo ambao
hufanya wizi wa maji kwa kukwepa
tozo ila wanapobainika hutozwa pesa nyingi na hatua nyingine za kisheria
huchukuliwa dhidi yao
Na
Rweikiza Katebalirwe Dodoma FM
Comments
Post a Comment