Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) inatumia Jumla ya shilingi milioni 485 kwa mwezi katika kuhakikisha huduma ya maji safi inawafikia kwa urahisi wakazi wa manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka mamlaka hiyo Bwana Sebastian Warioba
ameyasema hayo wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya mfumo mpya wa ulipaji wa bili ya maji
kwa njia ya simu.
Amesema
kiasi hicho cha fedha kimegawanyika katika maeneo tofauti ikiwemo ulipaji wa
nishati ya umeme unaotumika katika kuzalisha
na kusukuma maji hayo ili kuwafikia wananchi, malipo ya wafanyakazi
pamoja na marekebisho ya mitambo ya usafirishaji wa huduma ya maji.
Aidha
Bwana Warioba amesema (DUWASA) ndie mwenye jukumu la kufanya marekebisho ya
miundombinu ya maji pale inapoharibika lengo ikiwa ni kuendelea kutoa huduma
stahiki kwa wananchi na jukumu la mwananchi ni kutoa taarifa za uwepo wa
uharibifu wa miundombinu hiyo ili kufanyika marekebisho na kuokoa upotevu wa
maji.
Katika
hatua nyingine Bw. Warioba amesema ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi
mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa ulipaji wa kodi kupitia simu za kiganjani
mfumo ambao unarahisisha kumpatia mteja taarifa mbalimbali za matumizi ya
huduma ya maji.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment