Mdhibiti na Mkaguzi
mkuu wa hesabu za serikali Prof Mussa Juma Assad ametoa ufafanuzi juu ya uwepo
wa makosa katika ripoti ya ukaguzi ya
mwaka wa fedha iliyowasilishwa kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT
John Pombe Magufuli.
Akiongea na waandishi
wa habari hii leo prof Assad amesema kuwa mnamo March 27, mwaka huu
aliwasilisha ripoti zake za ukaguzi wa mwaka wa fedha ulioishia mnamo june 30/
2017 kwa rais Magufuli ambapo ripoti hizo zilikuwa na dosari juu ya mwenendo wa
deni la Taifa.
Amebainisha kuwa hadi
kufikia June 30, 2017 deni la Taifa lilikuwa shilingi tirioni 46.08 ambapo kati
ya deni hilo ,deni la ndani ni shilingi tirion 13.34 sawa na asilimia 29 na
deni la nje ni shilingi tirioni 32.75 sawa na asilimia 71 hivyo deni la nje ni
aslimia 31 ya pato la Taifa na kwamba kwa sasa deni la Taifa ni himilivu.
Akiendelea kutoa
ufafanuzi kufuatia kauli yake wakati wa uwasilishaji wa ripoti hizo prof Assad
ameomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi huku akidai kuwa matokeo
ya ukaguzi wa ripoti hizo yatawekwa wazi kwa umma baada ya kuwasilishwa
bungeni, tukio linalotarajia kufanyika kabla ya april 12 mwaka huu, katika
kikao cha kwanza cha bunge kitakachofanyika baada ya ripoti za CAG kuwasilishwa
kwa Mh Raisi.
Na Alfred Bulahya DODOMA
FM
Comments
Post a Comment