
Jumla ya shilingi bilioni 896.3
zimetumika kulipa madeni ya watumishi wa umma wakiwemo wakandarasi pamoja na
watoa huduma waliokuwa wakiidai serikali baada ya kukamilika kwa zoezi la
kuhakiki madeni ya watumishi wa umma katika awamu ya kwanza.
Msemaji mkuu wa
Serikali Dr. Hassan Abbas ameyasea hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofsini kwake Mjini Dodoma na kueleza kuwa adhima ya kulipa madeni hayo
inatokana na ahadi iliyotolewa na Rasi Dr. John Pombe Magufuli kulipa madeni
yote ya watumishi wa umma.
Amesema fedha hizo
ni kati ya shilingi Trilioni 1 iliyotengwa na Serikali kwa ajili ya
kushughulikia malipo ya watumishi wa umma wanaoidai serikali na baada ya
kuhakiki madeni hayo katika awamu ya kwanza, zoezi hilo linaendelea tena katika
awamu inayofuata.
Dr. Abbas amesema
Serikali inaendelea na uhakiki wa madai ya watumishi wa umma ili kuhakikisha
kuwa kila mtumishi anapatiwa stahiki yake na kila uhakiki utakapokuwa ukikamilika
taarifa itakuwa ikitolewa kwa vyombo vya habari na watumishi hao wakipatiwa
stahiki zao.
Katika hatua
nyingine Dr. Hassan Abbas amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ambapo mabehewa 1590
pamoja na vichwa vya treni 25 vimekwisha kuagizwa sambamba na ujio wa ndege nne
mpya hadi kufikia mwezi july mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa anga.
Na
Pius Jayunga Dodoma Fm Radio
Comments
Post a Comment