Skip to main content

BEKI SIMBA APATA AJALI YA PIKIPIKI, AENGULIWA SAFARI YA MISRI

                        Image result for salim mbonde simba 

AJALI ya bodabda imemuondoa kikosini beki wa Simba, Salim Mbonde baada ya kuondolewa katika kikosi kinachosafiri nchini kesho kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry, Kombe la Shrikisho Afrika.

  Simba itakuwa ugenini dhidi ya Al Masry katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Port Said mjini Port Said, Misri ikihitaji ushindi wowote kusonga mbele, baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumatano wiki iliyopita.

  Beki huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji walikuwepo katika mipango ya Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre kumtumia katika mchezo huo kutokana na ajali hiyo iliyosababisha ashonwe nyuzi tatu juu kidogo ya jicho, amemuondoa katika mipango hiyo.

 

bonde alisema hatakuwepo katika mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata katika ajari hiyo kwa kusababisha kushindwa kuendelea na mazoezi ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao.

 
“Sitakuwepo katika msafara huo, suala la kuanza lini mazoezi bado sijajua kwani bado sijatoa nyuzi nadhani baada ya kurejea nitaungana na wenzangu baada ya kupata taarifa kutoka kwa daktari wa timu,” alisema Mbonde.

 
Beki huyo wa kati, amekutana na majanga hayo baada ya kutoka katika majeruhi yaliyomuweka nje tangu Oktoba 15 mwaka jana alipoumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar

.
Kwa ujumla, Simba inawakosa mabeki wake wa kati waliounda ukuta imara mwanzoni mwa msimu, baada ya dirisha dogo pia kumuacha aliyekuwa Nahodha wake, Mzimbabwe, Method Mwanjali aliyekuwa anacheza pamoja na Mbonde.
Kwa sasa safu ya ulinzi ya Simba iliyopwaya inaundwa na chipukizi Yussuph Mlipili akishirikiana na ama na Erasto Nyoni, James Kotei au Juuko Murshid wakati mwingine – haina watu maalum bado.

 
Kikosi cha Simba kinaondoka kesho Alfajiri kwa ndege ya shiriki la Ethiopia, msafara ukiongozwa na Kaimu Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’.

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...