Baraza la biashara wilaya
ya bahi wameomba kupewa elimu zaidi juu ya mradi wa uboreshaji wa mazingira ya
biashara (LIC) ili kuwasaidia kuboresha biashaa zao.
Wajumbe hao wamesema elimu hiyo
ikitolewa na kuwafikia wananchi itasaidia kuweza kuboresha biashara zao pamoja
na kupendekeza kuundwa
kwa kikosi kazi kitakachosaidia kuandaa mafunzo na kuandika maandiko
ili kupata fedha za ufadhili.
Aidha wamesema licha ya wao kuwa na
elimu lakini wapo wananchi ambao elimu hiyo haijawafikia hivyo wao wakianza
kupewa elimu itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia wananchi wengine kwa urahisi
na kuweza kuendana na Tanzania ya viwanda
Kwa upande wake Afisa biashara Wilaya ya
Bahi Said Isike ametaja changamoto zinazowakabili katika
uibuaji wa biashara kwa mwananchi mmoja mmoja kuwa ni uandikaji wa
maandiko ya kuwawezesha kupata ufadhili,
jambo ambalo ameahidi kulisimamia.
Kwa upande wake Mratibu wa mabaraza ya
biashara Mkoa (TNBC) Joseph Nyaromba amewataka wajumbe hao kuona umuhimu
wa chombo hicho ambacho kinatambulika kisheria ili wakuze biashara
zao na hatimaye wamsaidie Mh.Rais John Magufuli kuweza kufikia uchumi wa
Viwanda.
Afisa mwandamizi wa huduma na elimu
kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma Barnabas
Masika amesema kama mamlaka wapo tayari kushirikiana na wilaya hiyo katika
kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha juu ya ufanyaji biashara zao.
Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment