
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma zimetajwa kuathiri miundo mbinu ya barabara
katika wilaya ya Chamwino kata ya Mvumi hivyo kupelekea kubomoka kwa daraja linalounganisha
barabara kutoka Mvumi kuelekea Dodoma mjini.
Hayo yamethibitshwa na kaimu katibu afisa tarafa wa
kata ya Mvumi Bwana Sospita Mwasuke wakati akizungumza na Dodoma FM ambapo
ameeleza kuwa barabara zote zimeharibiwa na mvua hali iliyolazimu wakazi
wanaoishi maeneo hayo kutumia usafiri wa
pikipiki kutokana na magari kushindwa kupita.
Aidha Bwana
Sospita amesema kuna idadi kubwa isiyojulikana ya nyumba pamoja na vyoo ambavyo
vimeanguka kutokana na mvua hizo.
Hata hivyo amewahimiza wakazi wa eneo hilo kuchukua
tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kuhakikisha miundo mbinu ya makazi kuwa
ya uhakika ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.
Na Benard Filbert DODOMA
FM
Comments
Post a Comment