Zoezi
la kuhamishwa kwa kituo cha mabasi Mkoa wa Dodoma na kupelekwa Nane nane Nzuguni
limeahirishwa kwa siku ya leo kutokana
na kukosekana kwa banda la kupumzikia abiria.
Mkurungezi wa
manispaa ya Dodoma Bwana GODWINE KUNAMBI amesema wamezungumza na shirika la
Reli na limewapa muda wa wiki moja ili kukamilisha mahitaji ya wadau ya
ukarabati wa miundombinu katika kituo cha Nane nane ikiwa ni pamoja na kuweka
mazingira katika hali ya usalama kwa abiria.
KUNAMBI ameongeza
kuwa tayari ameonana na wamiliki wa
mabasi , wadau mbalimbali wa kituo pamoja na mawakala na wamekubaliana kuhamia
Nane nane ili kupisha eneo hilo ambalo ni mali ya shirika ya reli kwa ajili ya
ujenzi wa reli.
Aidha Mkuu wa mkoa wa
Dodoma Dokta BINILITH MAHENGE amekutana na bodi ya maandalizi ya sherehe za Nane
nane TASO na kukubaliana kukaa katika eneo hilo huku wakisubiri ujenzi wa kituo
cha Mabasi cha Kisasa ambacho kitachukua takribani mwaka mmoja na miezi sita
kukamilika.
Dokta BINILITH
MAHENGE amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha imekuwa ni vigumu kuhamisha kituo hicho cha
mabasi kwa siku ya leo na kubainisha
kuwa eneo hilo halina banda la kijikinga na mvua kwa abiria.
Na
Mindi Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment