
Imeelezwa
kuwa wanajamii wamekuwa hawatambui haki
pamoja na wajibu wao juu ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo pamoja na
kuwa na uwazi na uwajibikaji katika kutoa huduma hususani za kiserikali.
Hayo yamebainishwa
na mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za kiraia mkoani Dodoma (NGONEDO) Bi, Sara Mwaga wakati akifungua mafunzo ya kujengea
uwezo asasi za kiraia Wilayani Chamwino
yenye lengo la kujenga uwazi na uwajibikaji kwa jamii na katika
kufuatilia na kuangalia maswala ya serikali za mitaa na taarifa mbalimbali za
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na utawala bora.
Bi Sara amezitaka
asasi za kiraia kutumia mafunzo hayo vizuri kwa kuongeza ufahamu na kupata
mbinu zitakazowawezesha kufanya kazi na kuwajibika katika kuliletea Taifa
maendeleo.
Kwau pande wake
Mratibu wa Asasi za kiraia Bw, Edrward Mbogo amesema kupitia asasi za kiraia
zitakazoshiriki mafunzo hayo ya siku mbili asasi hizo zitasaidia jamii kwa kupeleka
elimu waliyojifunza kwa vitendo huku akiishukuru serikali ya halmashauri ya Chamwino
kwa kuunga mkono mafunzo hayo.
Akizungumza katika
mafunzo hayo muwezeshaji kutoka chuo Kikuu cha Dodoma Dkt, Ajali Mustapha
amesema asasi za kiraia zinafanya kazi kwa niaba ya jamii inayowazunguka na
kwamba zinamchango mkubwa katika harakati za kiutawala, uwazi na uwajibikaji .
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kumekuwa na changamoto nyingi katika
jamii ikiwemo kutokutatuliwa changamoto zao kwa wakati kutokana na ufinyu wa
bajeti .
Na
Phina Nimrod
Dodoma FM
Comments
Post a Comment