Skip to main content

WATU 18 WAMEPOTEZA MAISHA MKOANI DODOMA KUTOKANA NA KUUGUWA UGOJWA WA KIPINDUPINDU

 

JUMLA ya watu18 wamepoteza maisha Mkoani Dodoma  kutokana na kuugua ugonjwa wa kipindupindu huku zaidi ya wagonjwa 400 wakiwa wanaugua ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa  Mjini Dodoma na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. JAMES KIHOLOGWE wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuwepo kwa ugonjwa wa Kipindupindu mkoani Dodoma.

Aidha Dk. KIHOLOGWE amesema kuwa ugonjwa huo wa mlipuko umeanza Mwezi Oktoba mwaka jana katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwamba ugonjwa huo upo zaidi katika wilaya za Mpwapwa na Chamwino  licha ya  kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuutokomeza ugonjwa huo.

Amebainisha kuwa hadi kufikia siku ya jana kulikuwa na jumla ya wagonjwa wapya 26 ambao waliongezeka Mkoani hapa huku wagonjwa  22 wakiruhusiwa.

 Hata hivyo Mganga mkuu ameeleza jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuutokomeza ugonjwa wa kipindupindu katika Mkoa wa Dodoma.

Pia  ametoa wito kwa wakazi  wote wa Mkoa wa Dodoma kuzingatia suala zima la usafi ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa na kunawa mikono kwa sabuni  wakati wa kula na wanapotoka kujisaidia.


Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...