
Wakulima mkoani Dodoma
wameshauriwa kulima kilimo cha umwagiliaji ambacho kitawaingizia kipato mbali
na kusubiri kilimo cha msimu wa mvua.
Ushauri huo umetolewa
na mwenyekiti wa kata ya mlowa wilayani chamwino Bw.Amosi Louna Wakati
akizungumza na taswira ya habari na kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji kinaweza
kumsaidia mtu kujiingizia pesa nyingi zitakazo msaidia kujikimu mahitaji yake
kwa kipindi chochote tofauti na kusubiri msimu wa mvua pekee.
Bw. Louna Amesema njia
rahisi ya kulima kilimo cha umwagiliaji ni pamoja na uvunaji wa maji kwa
kipindi cha kiangazi kwa kutumia njia mbalimbali za uhifadhi wa maji kama vile
uchimbaji wa visima pamoja na mabwawa makubwa yenye uwezo wa kukaa na maji kwa
kipindi cha masika.
Nae Afisa kilimo mkoani
hapa Bw. Benard Abrahamu amesema ili kuhakikisha mkulima anapata mazao
yanayoendana na maeneo waliyolima, wakulima wanatakiwa kushirikiana na maafisa
ugani katika kuhakikisha wanapatiwa huduma zitakazo fanya mazao kukua
pasipokushambuliwa na wadudu.
Sanjari na hayo
wakulima wametakiwa kufahamu kuwa kilimo ni uti wa mgongo na ni tegemezi kwa
jamii nzima hivyo watumie fursa hiyo kwa kubuni njia tofauti za kilimo bora ili
wajivunie kuwa wakulima.
NA ANIPHA RAMADHAN
Comments
Post a Comment