Skip to main content

SIASA ZINAATHIRI UTEKELEZA WA MIPANGO MIKAKATI YA ELIMU

 

Wadau wa elimu wamesema ili kufanikisha mikakati waliyojiwekea na itakayo inua kiwango cha elimu mkoani Dodoma  ni lazima kutoingiza siasa katika suala la elimu.
Katika kikao cha wadau wa elimu kilichodumu kwa siku mbili wamejadili njia za kuufanya mkoa wa Dodoma kukua kielimu ambapo moja ya wadau dr Fransis wiliam mhadhili kutoka chuo kikuu Dodoma amesema ili elimu iwezeze kukua ni lazima kuimarisha uwajibikaji na utendaji kazi kwa walimu.

Nae mwenyekiti wa chama cha waalimu mkoa wa dodoma mwal.augustine njamasi amesisitiza ili kukuza ufaulu ni lazima kuwaangalia waalimu kwa jicho la pekee na kutowachukulia waalimu kama wahalimfu pindi wanafunzi wanapofanya vibaya.


Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa dodoma dk binilith mahenge amesema  fursa za ujio wa makao makuu dodoma zitawahusu zaidi wasomi  hivyo amehimiza wananchi kuzingatia elimu ili kunufaika na furasa hizo

katika kikao hicho kilichoanza feb 20 na 21  kumetolewa tuzo ya vyeti na vikombe kwa wilaya zilizofanya vizuri na tozo ya bendera nyeusi kwa wilaya zilizofanya vibaya ambazo wilaya ya chemba iliyofanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba na wilaya ya bahi iliyofanya vibaya katika matokeo ya kidato cha nne na viongozi wa wilaya zote hizo waameahidi kufanya vizuri katika matokeo yajayo.

Mariam Matundu ………………………………chanzo Dodoma Fm

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...