
Waathirika wa
ugonjwa wa virusi vya ukimwi
wameshauriwa kujiunga na taasisi
mbalimbali za uzalishaji mali ili kuondokana na unyanyapaa na suala la
utegemezi.
Ushauri huo
umetolewa na mratibu wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi Manispaa ya Dodoma dokta
Elias Nyoni wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema ni vizuri waathirika wa virusi
vya ukimwi wakajiunga na taasisi mbalimbali ambazo zinajihusisha na uzalishaji
kiuchumi.
Dokta Eliasi
amesema kuna taasisi ambazo zinajihusisha na utoaji mikopo kwa waathirika wa
virusi vya ukimwi lengo likiwa ni kuwasaidia kupata kipato kutokana na baadhi
yao kukata tamaa na kujiona kama wananyanyapaliwa katika jamii.
Ameongeza kuwa
matatatizo ya kunyanyapaa watu wenye virusi vya ukimwi bado yapo na hali hiyo
hupelekea kuwakatisha tama waathirika hao huku akisema kuna baadhi ya
waathirika wanajiweza kiuchumi na kufanikiwa kufanya mambo makubwa ya
kimaendeleo katika jamii ikiwepo kuwapeleka watoto shuleni.
Akiongea na kituo
hiki mmoja wa wakazi mkoani Dodoma Bwana Fidelis Leonard amesema ni vibaya kwa
mtu yeyote kumnyanyapaa mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwani kwa
kufanya hivyo hujihisi ni mtu asie na haki sawa na wengine.
Msemaji wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Glory Mziray hivi karibuni alisema
Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi
(VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo
wa kubadili tabia.
Na
Benard Filbert Chanzo :Dodoma FM
Comments
Post a Comment