Shule ya Msingi
IBWAGA iliyopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa
matundu ya vyoo hali inayo wapa wakati mgumu wanafunzi hasa wa kike wawapo
katika kipindi cha hedhi.
Shule ya Msingi
IBWAGA inakabiliwa na uhaba wa vyoo
ambapo ina uhitaji wa jumla ya matundu ya vyoo 41 ambapo yaliyopo ni matundu 10
pekee .
Akiongea na Dodoma
fm Mwalimu Mkuu Msaidizi katika shule hiyo Mw. EDEFRIDA MZERU amesema kuwa vyoo
walivyo navyo ni vya muda mrefu na baadhi ya vyoo hivyo havina milango hali
inayowapa wakati mgumu wanafunzi wa kike wakati wa kujisaidia kipindi cha
hedhi.
Baadhi ya wanafunzi
wa kike katika shule hiyo wameiomba serikali
kuwasaidi kuondokana na changamoto hiyo
ya upungufu wa vyoo na kusema
kuwa hali hiyo imekuwa ikipelekea wakati mwingine kuchelewa kuingia darasani
kutokana na foleni iliyoko wakati wa
kwenda kujisaidia.
Hata hivyo Mwalimu
Mzeru amesema shule inajitahidi kuhakikisha inaondokana na changamoto waliyo nayo
ya uhaba wa matundu ya vyoo na kwamba tayari wamekwishaanza ujenzi wa chumba
kimoja kwa ajili ya choo kwa wanafunzi wa kike.
Na
Phina Nimrod Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment