
Katika kipindi cha
mwezi octoba mwaka 2017 hadi feb.2018 jumla ya watu wapatao 20 wamepoteza
maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mkoani Dodoma.
Afisa afya Manispaa
ya Dodoma Bw. Abdalha Mahiya ametoa takwimu hizo wakati akizungumza na kituo
hiki na kueleza kuwa Wilaya ya Mpwapwa inaongoza kwa maambukizi hayo ambapo
kati ya vifo vya watu 20, 18 ni kutoka Wilaya ya Mpawapwa huku wagonjwa 322
kati ya 471 wakitokea wilaya hiyo.
Amezitaja Wilaya nyingine
zinazoongoza kwa maambukizi hayo kuwa ni Kongwa, Bahi pamoja na Chamwino huku
akieleza chanzo kikubwa cha maambukizi hayo kuwa ni matumizi ya maji yasiyokuwa
safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Bw. Mahiya
amewasihi wananchi kuacha tabia ya kujisaidia hovyo bila kuzingatia matumizi
sahihi ya vyoo pamoja na utiririshaji hovyo wa maji taka jambo linalochangia
maambukzi ya vimelea vya ugonjwa wa kipindu pindu.
Hata hivyo kituo
hiki kimezungumza na baadhi ya wananchi wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao
wameonesha kushangazwa kutapakaa kwa biashara ya vyakula na matunda katika
maeneo ambayo sio rafiki kwa shughuli hizo na kuzitaka mamlaka husika kudhibiti uuzwaji wa vyakula katika maeneo
yasiyokuwa rafiki.
Na
Pius Jayunga Chanzo: Dodoma Fm
Comments
Post a Comment