Chama cha walemavu TOSODEFFA mkoani Dodoma kimeiomba serikali kuanzisha tena kwa mara nyingine vyuo vya walemavu ambavyo vilikuwa vimesitisha mafunzo yake ili kupunguza ongezeko la walemavu wanaoishi kwa kutegemea msaada.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Bwana Paul Manyika alipokuwa akizungumza na taswira ya habari ofisini kwake ambapo amesema kipindi cha awali kulikuwa na vyuo vingi vya walemavu nchini hivyo ilikuwa rahisi kwa walemavu kupata ujuzi mbalimbali na kujitegemea baada ya mafunzo lakini sasa hivi vyuo vimepungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia kuhusu ukosefu wa ajira kwa walemavu nchini amesema ni changamoto inayowakabili na kupelekea ongezeko la walemavu ambao wanaishi mtaani bila kazi wakati baadhi yao wana uwezo wa kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali.
Pamoja na hayo amesema ni vigumu kwa mtu mwenye ulemavu kupewa msaada mara kwa mara ili aweze kukidhi mahitaji yake hivyo kungekuwepo na vyuo hivyo vingesaidia kumuandaaa mlemavu kutokutegemea kuajiriwa na hatimaye kutegemea kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwepo ufundi selemala,pamoja na ujenzi.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi akiwepo bwana Kitavian Gaspar amesema ni vizuri serikali ikajenga vyuo hivyo ili kusaidia watu wenye ulemavyu kujikwamua kiuchumi.
Comments
Post a Comment