Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizo
fanikiwa kupunguza vifo miongoni mwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano .
Ripoti ya
vifo vya watoto wachanga iliyotolewa feb 20 mwaka huu na unicef inaonesha kuwa
watoto 25 katika vizazi 1,000 hufa kwa
mujibu wa utafiti wa demografia na afya
wa tanzani TDHS wa mwaka 2015/2016.
Usia ledama ni afisa mawasiliano wa unicef hapa
Tanzania amesema licha ya Tanzania kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka
mitano bado kunaidadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga na kina mama ambapo
takribani watoto elf thelathini na tisa wanafariki kila mwaka.
Amesema miongoni mwa watoto wanapoteza maisha
hutokana na magonjwa yanayozuilika ikiwemo maralia,homa ya mapafu na magonjwa
ya kuhara ambpo takribani watoto 270 wenye umri chini ya mika mitano wanapoteza
maisha kila siku na karibu vifo 6 hadi 10 hutokea katika siku yao yakwanza
wanapozaliwa.
Aidha amesema serikali ,taasisi na jamii inapaswa
kudhamilia kutoa huduma rahisi nafuu kwa wakina mama katika kupunguza vifo vya
watoto wachanga na kina mama wajawazito.
Shirika la kimataifa la kuwahudumia watoto duniani
unicef limezindua ripoti ya vifo vya watoto wachanga duniani pamoja na kampeni inayoitwa kila mtoto aishi
yenye lengo la kutoa suluhisho kwa watoto wachanga duniani.
Mariam
Matundu
chanzo Dodoma Fm
Comments
Post a Comment