Msanii na mtayarishaji wa mziki wakizazi kipya Salmoo kutoka more feelings
production amesema baadhi ya lebo zilizopo mkoani hapa zina msaada mkubwa kwa
wasanii kwani kuna utofauti mkubwa kwa sasa ukitofautisha na zamani.
Salmoo amesema hayo wakti akizungumza na Dodoama Fm Radio ambapo ameitaja
lebo ya biorn kuwa ni miongoni mwa lebo inayowasimamia wasanii vizuri.
Akizungumzia kuhusu ukuaji wake katika kutayarisha mziki amesema
kumechangiwa na producer mwenzake melodies ambaye amehusika kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo amesema msanii hutakiwi kutegemea kufanya staili moja ya mziki
ila unatakiwa kuwa kila upande.
Hivi karibuni msanii huyo ameachia kazi yake mpya inayoitwa my wife
aliyomshirikisha jacobeat ambapo amesema anafanya utaratibu wa kushoot video
hadi kufika mwezi wa tatu itakuwa tayari.
Comments
Post a Comment