Mwenyekiti wa chama cha
Act-Wazalendo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Masudi Bigangika amekanusha
uvumi wa taarifa zilizokuwa zinamhusisha kukihama chama hicho na kujiunga na
chama cha Mapinduzi (CCM).
Bw. Bigangika ameyasema
hayo wakati akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu kufuatia uvumi ulioanza
kuenezwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi Wilayani humo kuwa
mwenyekiti huyo amekihama chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi.
Amesema kuwa taarifa zilizotolewa
na baadhi ya viongozi wa CCM Wilayani humo ni uvumi unaosambazwa kwa lengo la
kumchafua yeye na chama chake licha ya kuwa yeye hayupo tayari kukihama chama
chake cha ACT Wazalendo.
Aidha Bw. Bigangika
amesema kutokana na wimbi la viongozi mbalimbali kuhamia chama cha mapinduzi
huwenda ikawa ni moja ya sababu za kuzushwa kwa uvumi wa yeye kukihama chama
chake na kukiri kuwa kutokana na kuenezwa kwa taarifa hizo kunaweza kuchangia
kwa sehemu kubwa kudhoofisha wafuasi wa chama cha ACT wazalendo
Katika hatua nyingine
Bw. Bigangika ametoa Wito kwa wananchi na wafuasi wa chama cha Act wazalendo
kupuuza taarifa zinazotolewa na watu katika mitandao ya kijamii na badala yake
watu wajenge mazoea ya kusikiliza kauli ya kiongozi husika ili kuepuka
mkanganyiko miongoni mwa jamii.
Comments
Post a Comment