Serikali
imewataka maafisa elimu kote nchini kutowaficha waalimu wanaofanya vitendo
viovu dhidi ya wanafunzi bali kuwabainisha ili wachukuliwe hatua kwa
mujibu wa sheria.
Hayo yameelezwa hii leo mjini Dodoma na waziri wa
nchi,ofisi ya rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo
wakati akifungua kikao cha kazi cha siku mbili cha maafisa elimu wa
mikoa na wilaya chenye lengo la kujadili
mipango,malengo na mikakati ya uboreshaji elimu nchini.
Waziri Jafo amewaeleza kuwa haridhishwi na baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi kwani jambo hilo si tu
linakiuka maadili bali pia ni chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Kupitia kikao hicho imemlazimu waziri Jafo kumuagiza naibu katibu mkuu wa TAMISEMI kuchunguza na kufanya maboresho ili mkoa wa Dodoma ambao ndio makao makuu ya nchi uweze kufanya vizuri
Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mussa Iyombe amewataka maafisa elimu kujitathimini iwapo wanaiweza kazi hiyo na kuacha tabia ya kuwatesa waalimu bali kutatua changamoto zao.
Kufuatia maagizo hayo mwenyekiti wa maafisa elimu wa mikoa na wilaya Mayasa Hashimu amesema kuwa watatekeleza maelekezo yote na kuahidi kutoka na maazimio ya kiutendaji katika kikao hicho.

Mariam
Matundu
Comments
Post a Comment