Kina mama Wilayani Kongwa wametakiwa kufika katika vituo vya afya ili kupata maelekezo sahii juu ya matumizi ya njia bora za uzazi wa mpango kutokana na baadhi yao kutokuwa na uelewa.
Akiongea na Dodoma FM Afisa Muuguzi na Mratibu wa Uzazi wa Mpango wa Wilaya ya Kongwa Bi. Lessy Mdegellah amesema wapo baadhi ya kinamama ambao wamekuwa wakisikia maneno ya upotoshaji kutoka kwa watu wasiokuwa na ufahamu juu ya njia za uzazi wa mpango hivyo amewataka kuondoa uoga na kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kupata maelekezo ya kitaalam.
Bi. Lessy amesema yapo maudhi madogo madogo kwa baadhi ya kina mama wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambayo huisha baaada ya muda mfupi na kuwataka kina mama watakaokutana na maudhi hayo kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya.
Sambamba na hayo Bi. Lessy amesema zipo faida mbalimbali za kutumia njia za uzazi wa mpango ikiwemo kumpa mama na baba nafasi ya kufanya shunghuli nyingine pamoja na kumpa mtoto nafasi ya kukua vizuri.
Wakizungumzia faida za kutumia njia za uzazi wa mpango baadhi ya kina mama wamesema kuwa zinawapa nafasi ya kuzaa kwa mpangilio pamoja na kuondokana na changamoto ya kuwa na watoto wengi waliofuatana kwa umri.
Wito umetolewa kwa baadhi ya kina baba wanaowakataza wake zao kutumia njia za uzazi wa mpango kuwaruhusu ili kuwapa nafasi ya kupumzika.
Na Phina Nimrod Chanzo:Dodoma Fm
Comments
Post a Comment