Skip to main content

'KAPTENI' HIMID MAO AREJEA KUONGEZA NGUVU AZAM FC BAADA YA KUPONA


                         Related image 

WACHEZAJI wawili wa Azam FC, Nahodha Himid Mao ‘Ninja’ na mshambuliaji Wazir Junior, wamerejea rasmi mazoezini jana baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu wakiuguza majeraha yanayowakabili.

  Himid alikuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya goti la mguu wake wa kulia huku Junior akikabiliana na tatizo kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia, na tayari nyota hao wameanza kupata nafuu na sasa wanamalizia programu ya mazoezi mepesi kabla ya kuruhusiwa kurejea rasmi katika ushindani.

  Nyota hao wamerejea wakati kikosi cha Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) kikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Singida United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.

Junior anayetakiwa kufanya programu hiyo ya mazoezi mepesi kwa muda wa wiki moja, alisema anamshukuru Mungu kurejea tena dimbani huku akikiri kuwa ‘amemiss’ kucheza mpira.

 
“Kikubwa ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudi tena na nitaendelea kujituma kama ilivyokuwa awali kutokana na majeruhi haya ndo ilikuwa hivyo lakini tutapambana kama ilivyokuwa mwanzo, nimeumiss sana mpira nimemiss sana kucheza mpira na kuonyesha vile mashabiki wanataka.

 
“Lakini naamini kwa rehema za mwenyezi Mungu tutakaporejea tena basi mashabiki watafurahia vile walivyokuwa wakivisubiria,” alisema Junior
Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na wa aina yake kutokana na ushindani wa timu hizo uliokuwa kwa siku za hivi karibuni, tokea Singida United irejee Ligi Kuu msimu huu, ambapo katika mtanange wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...