Jamii imetakiwa kutambua utoaji wa elimu kwa watanzania juu ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya ni wajibu wa kila mtu ili kuondoa tatizo hilo nchini.
Akizungumza na kituo hiki sajent Cristian Mlelwa kutoka jeshi la polisi kitengo cha madawa ya kulevya mkoa wa Dodoma amesema kila mtu anawajibu wa kuelimisha jamii kuhusu kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya ili kuongeza elimu katika jamii.
Sajent Cristian amesema wao kama jeshi la polisi wanawajibika kwa nafasi yao kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu kuhusu madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya.
Hata hivyo amesema katika sehemu ambazo wanaenda kutoa elimu ikiwepo mashuleni wamekuwa wanawatumia waathirika wa madawa ya kulevya kama mfano kuonesha kuwa wameacha madawa ya kulevya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa vituo vya soba house nchini na aliyewahi kuwa muathirika wa madawa ya kulevya Bi Nuru amesema vituo vya soba house vilivyopo nchini vinamsaada mkubwa kwa waathirika
Bi Nuru ameongeza kuwa tarehe 24 mwezi wa pili wameandaa mchezo wa mpira wa miguu utakaofanyika uwanja wa jamhuri mkoani hapa ambapo kutakuwa na uchangiaji wa damu.
Comments
Post a Comment