Jamii imetakiwa kutambua mchango wa mwanamke katika kuelekea Tanzania ya wiwanda na uchumi wa kati kwani mwanamke anaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kuendeleza viwanda.
Wasomi kutoka katika chuo kikuu cha kikatoriki cha Ruaha kilichopo mkoani Iringa wamekiambia kituo hiki kuwa mwanamke iwapo akipewa nafasi na kutokukandamizwa na mfumo dume anaweza kuendeleza azma ya Tanzania ya viwanda.
Wamesema wanawake wengi wamekuwa wakithubutu kujituma katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani na kwamba iwapo watapata uwezeshwaji wa kutosha wataleta mchango mkubwa katika Tanzania ya viwanda.
Aidha wamesema kuwa jamii inapaswa kuachana na mila na desturi kandamizi kwa mwanamke na kwamba elimu inapaswa kutolewa hususani katika maeneo ya vijijini ambako ndio wahanga wakubwa wa vitendo vya mfumo dume.
Serikali imekuwa ikimpa kipaumbele mwanamke katika harakati za kuelekea Tanzania ya viwanda na hata kutumia kaulimbiu zinazoihamasisha jamii kutambua mchango wa mwanamke katika kuelekea nchi ya wiwanda na uchumi wa kati katika maadhimisho mbalimbali.
Comments
Post a Comment