Serikali imesema idadi ya watu walio na matatizo ya akili Nchini inakadiliwa kufika asilimia 1 na hii ni kutokana na wengi wao kuto kuhuduria katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu hatua inayochangia kukosekana kwa takwimu sahihi za idadi ya wagonjwa hao.
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Faustine Ndungulile ameyabainisha hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali Mbunge Joseph Mbona Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini alietaka kufahamu ni kwanini Serikali haina utaatibu wa kuwachukua wagonjwa wa akili mitaani na kuwapeleka katika hosptali za wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu.
Amesema watu walio na matatizo ya akili kwa sehemu kubwa asilimia 48 wamekuwa wakienda kupatiwa huduma katika vituo vya afya, asilimia 24 wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji na walio baki hupelekwa katika tiba za kiroho makanisani na mikisikitini huku wengine wakionekana mtaani bila kuwa na msaada wowote.
Amesema sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 inawataka ndug, na jamii kuwaibua watu walio na magonjwa ya akili na kuwapeleka katika vituo vya kutolea matibabu kwa usimamizi zaidi ili kupatiwa matibabu huku sheria hiyo ikiweka bayana kuwa afisa wa polisi, afisa usalama, afisa ustawi wa jamii Wilaya pamoja na viongozi wa dini wanawajibu wa kumbainisha mtu yeyote anaelanda landa na kutishia amani na usalama ili kumfikisha katika vituo vya afya
Katika kikao hicho Mbunge Halima Bulembo amesema si kila mgonjwa wa akili analanda mitaani na kushauri Serikali kufanya utafiti yakinifu ili kupata takwimu sahihi za wagonjwa wa akili Nchini kwa kuzingatia takwimu za shirika la afya Duniani WHO.
Comments
Post a Comment