
Moto mkubwa uliwaka hapo jana katika jengo la Hospital ya Aga Khani
(Apolo Medical Centre) Mkoani Dodoma na kuteketeza baadhi ya mali huku chanzo
cha moto huo kikielezwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza wakati wa zoezi la uokoaji na uzimaji wa moto huo Kamishina
Msaidizi wa Jeshi la zima moto na uokoaji Regina Kaombwe amesema walipokea
taarifa za moto huo majira ya saa kumi na moja kasorobo jioni ambapo kwa haraka
waliwahi eneo la tukio na kukuta jengo lote likiwa linawaka moto hivyo kuanza
kuudhibiti .
Baadhi ya wahusika kutoka katika hospital hiyo wakiwemo wafanyakazi
wamelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kuwahi eneo la tukio kadri ya
uwezo wao licha ya vitu vingi kuteketea kwa moto.
Mashuhuda ambao ni wakazi na wafanyabiashara wa maeneo hayo wamesema
walianza kuona moshi mkubwa katika hospital hiyo ndipo moto ukawaka.
Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Mkoani Dodoma lilifanikiwa kuuzima moto huo na hadi sasa haijajulikana
thamani ya vitu vilivyoteketea huku jeshi hilo likitoa wito kwa wananchi pindi
waonapo matukio ya moto kutoanza kuuzima taratibu bali wawasiliane na jeshi
hilo kwa kupiga simu namba 114 kwa ajili ya uokozi.
Mariam matundu Chanzo Dodoma Fm
Comments
Post a Comment