Kutokana na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto kutokukata bima zinapoisha kwa wakati Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA imekuja na mkakati wa kukomesha vitendo hivyo.
Bi Stela Rutaguza ni
meneja wa mamlaka ya usimamizi wa bima TIRA kanda ya kati amesema kuna baadhi
ya watu wamekuwa wakitengeneza bima feki hivyo amewatahadharisha kuwa iwapo
watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema wameanza zoezi
la ukaguzi wa bima katika vyombo vya moto mkoani hapa ili kubaini wenye bima
feki na kwamba zoezi hilo litakua ni endelevu na watakao bainika watafikishwa
mahakani kwa kufunguliwa kesi hivyo amewataka watumiaji wa vyombo vya moto
kuona umuhimu wa kuwa na bima zilizo halali.
Baadhi ya Wakazi wa manispaa
ya Dodoma na watumiaji wa vyombo vya moto wamesema zipo baadhi ya kampuni
zinazotengeneza bima feki ambapo wameiomba serikali kuendelea kufanya ukaguzi
ili kubaini wahalifu hao
Bima katika vyombo vya
moto ni muhimu katika kumlinda mtumiaji pale anapopata matatizo katika chombo
ikiwemo kumlinda kwa kupata stahiki zake pale anapopata ajali au kupotea kwa
chombo cha moto hivyo kuna kila sababu ya kupiga vita uwepo wa bima feki.
Mariam Matundu Chanzo Dodoma FM
Comments
Post a Comment