Ligi ya mkoa
wa dodoma inatarajia kuanza kutimua vumbi siku ya ijumaa feb 24 baada ya ratiba
ya ligi hiyo kutoka rasmi hapo jana ambapo mechi nne zitaanza kuchezwa katika
viwanja vya ccm jamhuri na ccm mgambo wilayani mpwapwa.
Ratiba hiyo
inaoneshwa kuwa Timu kutoka wilayan kondoa Ajax fc ambapo wapo kituo cha dodoma mjini
watacheza saa nane kamili mchana dhidi ya timu ya Dom city kutoka zuzu hku
jioni kukiwa na mchezo baina ya Derby ya Chamwino ya zamani Ila kwa sasa kila
timu ipo kata yake ,Gwasa nato kutoka chang'ombe wakicheza na Sheli Fc matajiri
kutoka chamwino katika mchezo wa jioni tarehe 23.
Wakati katika
kituo cha Mpwapwa kutakuwa na michezo miwili ambayo itapingwa katika dimba la
CCM mgambo kwa muda husika wa saa nane kwa mchezo wa kwanza na saa kumi kamili
jioni kwa mchezo wa jioni.
Ligi ya mkoa
wa dodoma ilitarajia kuanza mwezi wa
kwanza lakini kutoka na vilabu shiriki kushindwa kutekeleza kwa wakati vigezo
vya chama cha soka dodoma Pamoja na Tff imepelekea kuchelewa kwa ligi hiyo.
Na Selemani Juma Kodima
Comments
Post a Comment