Skip to main content

DODOMA: SOBA HOUSE YAOKOA MAISHA YA VIJANA 142

 

Kituo cha soba house kilichopo Mkoani Dodoma kimefanikiwa kutoa huduma ya matibabu kwa waraibu wa matumizi ya dawa za kulevya wapatao 142 huku vijana 98 kati yao wakiendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
Hayo yamesema na mratibu wa soba house Mkoa wa Dodoma Bw. Kwame Mhina wakati akielezea mkakati unaofanywa na kituo cha soba house Mkoani Dodoma katika kuwasaidia vijana waliokwisha kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema kituo cha soba house Mkoani Dodoma kilianzishwa tangu mwaka 2016 kikiwa na lengo la kuokoa nguvu kazi ya Taifa hasa kwa vijana walio kwisha kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya wakiwemo wale ambao bado hawajajihusisha na dawa za kulevya ili kuwaelimisha juu ya madhara yake.

Bw. Mhina amesema mwitikio kwa waraibu wa dawa za kulevya umekuwa mdogo kujitokeza kupatiwa ya kinga ya matumizi ya dawa za kulevya kutokana na watu hao kujenga hofu ya kuachishwa utumiaji wa dawa za kulevya na kupitia kituo cha soba house matarajio yao ni kuwafikia vijana wote waliokwisha kuathirika.

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakizungumza na kituo hiki juu ya mchango wao katika kuunga mkono juhudi za kupinga matumizi ya dawa za kulevya wamesema serikali inapaswa kaweka mkakati wa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya ili iwe rahisi kwa waraibu hao kujitokeza wao wenyewe.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa alikaririwa ikisisitiza wananchi kuacha kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kutokana na madhara yake kiafya na kwamba ipo adhabu kali kwa mtu anaebainika kujihusisha na biashara hiyo.
Na Pius Jayunga                                                                           

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...