
Wawakilishi wa kanda ya ziwa kunako Ligi soka wanawake nchini Tanzania kutoka jijini Mwanza Alliance Girls wamesema kuwa wamejipanga vilivyo kwenda kufanya kweli kunako ligi soka ya wanawake hatua ya nane bora ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 24 mwezi huu
Hayo yamesemwa na kocha wa klabu hiyo Ezekiel Chobanga wakatia akizungumza na michezo ya dodoma mapema leo Ambapo amesema wamejipanga kwenda kufanya vema katika mchezo wao wa kwanza jijini dar es salaam.
Amesema licha ya kutarajia kuanza kushiriki ligi hiyo lakini bado changamoto kubwa ambayo inawakabili ni Ratiba kuwabana kutoka na kushiriki mechi ya kwanza dar es salaam ,Mwanza na hatimaye ten Dodoma
Naye Nahodha wa timu hiyo ameelezea namna walivyojipanga yeye pamoja na wachezaji wenzake kuelekea nane bora ya ligi ya soka upande wa wanawake ambayo inatarajia kuanza mwezi wa pili tarehe 24 .
Kwa upande mwingine Amesema kuwa jamii wamekuwa wakitoa ushirikiano kwakuhakikisha watoto wa kike wanashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu.
Na Selemani Juma Kodima
Comments
Post a Comment