Maziwa ya
mwanzo ya mama yanatajwa kuwa na virutubisho vingi ambavyo ni muhimu kwa afya ya
mtoto mara baada ya kuzaliwa.
Dr. Abdalha Pumzi kutoka kitengo cha afya ya mama na mtoto katika
Hospitali ya Rufaa Mkoani Dodoma ameyabainisha hayo wakati akizungumza na kituo
hiki kuhusu faida za maziwa ya mwanzo kwa mtoto mara baada ya mama mjamzito kujifungua.
Amesema maziwa yanayotoka baada ya mama mjamzito kujifungua husheheni
protin na vitamini “A” kwa wingi kutokana na vitamini hizo kuwa na uhitaji
mkubwa kwa mtoto na kwamba maziwa ya mwishoni huwa na idadi kubwa ya maji hivyo
kukamlia chini maziwa ni kumnyima mtoto virutubisho muhimu.
Dr. Pumzi amesema wapo baadhi ya wakina mama wamekuwa na tabia ya
kunyonyesha mtoto ziwa moja kwa kipindi kifupi na kumhamishia ziwa jingine
kitendo ambacho husababisha mtoto kupata protini, mafuta, pamoja na vitamini
kwa wingi na kukosa maji ya kutosha hivyo husababisha mtoto kupata choo kigumu
na wakati mwingine kukosa choo.
Pamoja na hayo Dr. Pumzi amesema suala la kuitunza afya ya mama na mtoto
ni jumuku la jamii kwa ujumla kuhakikisha mama na mtoto wanapatiwa mahitaji
yote muhimu ikiwemo lishe bora, kupata muda wa kupumzika pamoja na wazazi wote
wawili kuhudhuria Klinic kwa pamoja.
Na Pius
Jayunga Chanzo: Dodoma Fm
Comments
Post a Comment