Wadau wa elimu
wameombwa kushirikiana kwa pamoja kuinua elimu kwa mtoto wa kike ikiwa ni
pamoja na kuwa na miundombinu bora ya
vyoo ambayo itamuwezesha mtoto wa kike
kujistiri vizuri hasa katika kipindi cha hedhi.
Akizungumza na kituo
hiki mwalimu mlezi wa wanafunzi wa kike
kutoka shule ya sekondari kintiku Wilayani manyoni Maisala Mawala amesema kuwa tatizo la kukosa miundombinu
bora ya vyoo kunapelekea wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo kikamilifu hasa
wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Kwaupande wake makamu
mkuu wa shule hiyo Othumani Bakari amesema kuwa ili kuinua elimu kwa mtoto wa
kike jamii inapaswa kuwajibika kuondoa vikwanzo vinavyomfanya mwanafunzi wa
kike kushindwa kufanya vizuri katika masomo.
Baadhi ya wanafunzi wakike
kutoka katika shule hiyo wamesema hali ya kukosa miundombinu bora ya vyoo
katika shule yao inawafanya wasiwe huru pindi wanapokuwa katika siku za hedhi
hali inayopelekea kushindwa kusikiliza kwa makini na kuelewa wawapo darasani.
Comments
Post a Comment