Imeelezwa kuwa zaidi ya
asilimia sabini ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani mkoani Dodoma
wanatoka katika mikoa jirani huku wakidai ugumu wa maisha na manyanyaso ni
miongoni mwa sababu zinazowafanya wakimbie makwao.
Hamisi Ndoje ni afisa
ustawi wa jamii kutoka shirika linalo wahudumia watoto wanaoishi na kufanya
kazi mtaani kisedeti amesema sababu hizo zinapelekea watoto kuamua kuanza
kujitafutia mahitaji yao muhimu hali inayopelekea kujikuta wanaishi mitaani.
Aidha amesema kuwa
katika kipindi hiki serikali kuhamia
dodoma , watoto wanaona ni fursa wakiamini ongezeko la watu litawawezesha
kuomba na kupata msaada na hivyo wanakutana na watoto wengi wanaoishi na
kufanya kazi mitaani kutoka mikoa ya shinyanga ,mwanza,na Iringa .
Amesema ipo haja kila
mtu kubeba jukumu lake na kuwajibika ipasavyo ili kuepukana na visababishi
vinavyopelekea watoto wanaotoroka nyumbani na kwenda kuishi na kufanya kazi
mitaani.
Comments
Post a Comment