Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira mh, January Makamba amezindua Kamati ya taifa ya ushauri wa mazingira mkoani Dodoma
Waziri wa nchi ofisi ya
makamu wa raisi muungano na mazingira mh, January Makamba amezindua Kamati ya
taifa ya ushauri wa mazingira mkoani Dodoma lengo ikiwa kuishauri serikali
kuhifadhi na kuendeleza mazingira nchini.
Akizungumza na
wanahabari waziri January Makamba amesema kamati hiyo ina wajumbe mbalimbali
kutoka serikalini akiwepo mkurugenzi wa misitu,mipango miji na wengine ili
kuweza kuwapa ushauri wa kitaalamu waziri mwenye dhamana.
Amesema kwa kipindi
kirefu ambapo kamati hiyo haijakutana kuna uharibifu mkubwa wa mazingira katika
sehemu mbalimbali nchini huku viongozi mbalimbali wa kisiasa wakitoa matamko na
maamuzi mbalimbali kuhusu mazingira pasipo utaalamu.
Hata hivyo amezitaka
taasisi na wizara mbalimbali nchini kuitumia kamati hiyo juu ya masuala
yanayohusu mazingira ambapo kamati hiyo inawajibu wa kuita wizara yoyote na
kupokea taarifa juu ya uhifadhi wa mazingira katika sekta husika.
Wadau wa elimu
wameombwa kushirikiana kwa pamoja kuinua elimu kwa mtoto wa kike ikiwa ni
pamoja na kuwa na miundombinu bora ya
vyoo ambayo itamuwezesha mtoto wa kike
kujistiri vizuri hasa katika kipindi cha hedhi.
Akizungumza na kituo
hiki mwalimu mlezi wa wanafunzi wa kike
kutoka shule ya sekondari kintiku Wilayani manyoni Maisala Mawala amesema kuwa tatizo la kukosa miundombinu
bora ya vyoo kunapelekea wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo kikamilifu hasa
wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Kwaupande wake makamu
mkuu wa shule hiyo Othumani Bakari amesema kuwa ili kuinua elimu kwa mtoto wa
kike jamii inapaswa kuwajibika kuondoa vikwanzo vinavyomfanya mwanafunzi wa
kike kushindwa kufanya vizuri katika masomo.
Baadhi ya wanafunzi wakike
kutoka katika shule hiyo wamesema hali ya kukosa miundombinu bora ya vyoo
katika shule yao inawafanya wasiwe huru pindi wanapokuwa katika siku za hedhi
hali inayopelekea kushindwa kusikiliza kwa makini na kuelewa wawapo darasani.
Comments
Post a Comment