Shirika la Lead
Foundation linalojihusisha na utoaji wa
elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira kwa kufufua visiki imezindua mradi
wa kisiki hai Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya
mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya
nchi.
Akizungumza na wadau
mbalimbali wa mazingira wakati wa ufunguzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kongwa Mkurugenzi wa Shirika la Lead Foundation NJAMASI CHIWANGA
amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki hai ni kuhakikisha wanafikia Jumla ya
kaya laki moja na 80 ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira pamoja na
kustawisha miti milioni 14.
Njamasi amesema kuwa
mikakati waliyonayo katika mradi huo ni kujenga mshikamano wa wadau wote wa
mazingira pamoja na viongozi wa dini ili kushirikiana katika kufanikisha
kukomboa mazigira na wanatarajia kufikia tarafa mbili katika kila wilaya ili
kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake Mgeni
Rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deo Ndejembi amesema
anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa
ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.
Kwa upande wao baadhi
ya wadau waliofika katika ufunguzi wa mradi huo wamesema kuwa mpango wa kisiki
hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda
mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya kongwa itakuwa ni
historia.
Kisiki hai ni mradi wa
miaka
mitatu na unatarajiwa kufikia wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwa sasa
umenza na Wilaya ya Kongwa ambapo umeanza na tarafa ya Kongwa na Mlali katika
wilaya ya Kongwa.
Comments
Post a Comment