DK MEDARD KALEMANI AMETAKA TANESCO KUHAKIKISHA WANAONGANISHA UMEME KWA WATEJA WALIO LIPA KABLA YA MWAKA 2018
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amelitaka shirika la umeme
nchini Tanesco, kuhakikisha wananchi wote ambao wamelipia gharama za kuunganishiwa
umeme wanafanyiwa hivyo kabla ya mwaka huu haujamalizika na kuwapa agizo
mameneja wote wa shirika hilo nchini.
Waziri Dk. Kalemani ametoa agizo hilo wakati
akiwahikikishia wanakijiji wa muungano wilaya ya chamwino mkoani Dodoma kupata
umeme wa REA kabla ya mwaka huu haujamalizika ikiwa ni moja ya vijiji 33
vitakavyounganishiwa nishati hiyo.
Amesema kuanzia sasa mteja ambaye tayari amelipia gharama za
kuunganishia umeme, tanesco wanatakiwa kuunganishia ndani ya siku saba na wale
ambao wamelipia ndani ya mwaka huu wanatakiwa waunga nishiwe umeme kabla ya
mwaka huu haujaisha.
Awali mbunge wa jimbo la Mtera, Mh. Livingstone Lusinde, ambaye
ameshiriki katika ziara hiyo na waziri Dk. Kalemani, amesema umeme katika
baadhi ya vijiji vya jimbo lake kikiwemo kijiji cha Muungano ni shida hivyo
kuomba awamu hii ya tatu ya mradi wa REA kuwaanganishia na kuwawekea transfoma
yenye uwezo mkubwa.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Muungano wameeleza
umuhimu wa umeme watakapounganishiwa kijiji humo.
Comments
Post a Comment