Takwimu zinaonesha kuwa
takribani asilimia 61 ya eneo la nchi ya Tanzania lipo katika hatari ya kugeuka
kuwa jangwa huku mkoa wa Dodoma ukiwa ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika kwa
kiasi kikubwa.
Hayo yamesemwa na makamu wa
Rais Mh Samia Suluhu Hassani wakati
akizindua kampeni ya kuboresha mazingira eneo la Mzakwe katika mkoa wa Dodoma
kampeni inayofahamika kama kukijanisha Dodoma .
Amesema kampeni ya kuufanya mji
wa Dodoma kuwa mji wa kijani itakuwa kuvutio kwa watu na kuwavutia kuhamia makao makuu ya nchi.
Amesema wakati umefika wakazi
wote wa Dodoma kuhakikisha wanapanda miti miwili kwa kila kaya ili kuweza
kuifanya makao makuu Kuwa yenye mvuto.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi yaM wa Rais muungano na mazingira
Mh,January Makamba amesema kampeni ya kuifanya makao makuu iwe ya kijani
kupitia upandaji wa miti itakuwa endelevu ili kuleta mandhari inayotakiwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma
Dk Binilith Mahenge aliyewahi kuwa
waziri wa mazingira amesema kampeni ya upandaji miti ilianza mwaka 2006 huku
akiwaomba watanzania kuhakikisha wanapanda miti pamoja na kustawisha.
Kampeni ya kuboresha mazingira
ambayo imezinduliwa na makamu wa Rais imeambatana na kauli mbiu isemayo DODOMA
YA KIJANI NDO MPANGO MZIMA.
Comments
Post a Comment